About Me

header ads

KILIMO CHA KOROSHO

KILIMO BORA CHA KOROSHO : Korosho ni zao ambalo chimbuko lake ni Portuguese na baadae katika karne ya 16 ndipo lilipofika africa katika nchi ya msumbiji na baadae likafika nchini Kenya na Tanzania.

Kwa hapa Tanzania korosho hulimwa na kustawi vizuri katika mikoa ya kusini Mtwara, lindi, na maeneo kama Mafia, bagamoyo na Rufiji.

KIWANGO CHA MVUA ;

Korosho hustawi vizuri kwenye maeneo yenye mvua 840mm – 1250 mm wastani wa mvua kwa mwaka,napia hukua vizuri kwenye maeneo 0- 500 m kutoka usawa wa bahari.

UDONGO UFAAO KWA KILIMO HIKI ;

Korosho ukua vizuri kwenye maeneo yenye PH 5.6 udongo wa kichanga (sandy) na pia udongo mfinyazi kichanga.

KUANDAA SHAMBA

Kama mazao mengine shamba la korosho linatakiwa kusafishwa, kusawazishwa nakutifuliwa vizuri kwaajili ya kupanda korosho.

nakatika mashimo utakayo chimba unaweza kuweka mbolea ya ngombe ukachanganya na udongo mapema ili kuongeza rutuba.

KUPANDA

Ni muhimu sana kuchagua mbegu bora kwa kua mbegu utakayo panda ndo itakuonesha kiasi gani utavuna, baada ya kununua mbegu unachukua maji na chumvi 100g ya chumvi unaweka katika maji kiasi cha lita 5 unakoroga vizuri na unachukua mbegu zako unaweka kwenye maji hayo zile zitakazo zama ndio mbegu zenye uwezekano mkubwa wa kiota, baada ya hapo unazianika vizuri hili ziweze kukauka.

KUNA AINA MBILI ZA UPANDAJI WA KOROSHO AMBAZO NI :

Kupanda moja kwa moja ; hii ni njia mambayo ni risk sana na inaitaji umakini kwa sababu kunauweze3kano mkubwa wa mbegu kufa. ukitumia njia hii unatakiwa kupanda mbegu tatu 3 katika shimo moja na baada ya miezi mi 3 – 4 ngoa mimea na bakiza mmoja wenye afya na muonekano mzuri.

Njia ya kitaru ; hii ni njia ya pili na ni nzuri kwa sababu unakua huru kuchagua mche ambao umestawi na ulio na muonnekano mzuri , unatakiwa kuamishia miche shambani ikiwa na umri wa wiki 6 na zingatia kuchagua mche wenye afya.

Na baadae unatakiwa kupunguza majani urefu wa sm60- 90 kutoka kwenye ardhi na pia ondoa majani yote ambayo yanaonekana kuadhiliwa na magonjwa au wadudu na yale yalio kauka.



MAGONJWA NA WADUDU

MAGONJWA

Anthracnose·

powdery mildew·

hayo ni magonjwa yanayo athiri sana korosho



WADUDU

Cashew stem girdler·

Cashew weevil·

Coconut bug·

Heliotropes bug·

Meal bug·

Trips aphids·



NAMNA YA KUZUIA WADUDU NA MAGONJWA

Ili kuzuia magonjwa na wadudu unatakiwa

 Palilia mapema

 Weka shamba katika hali ya usafi

 Tumia mbinu ya kuchanganya mazao kwa korosho unaweza kuchanya pamba au maharage hiyo inasaidia kukimbiza wadudu wengine ambao wanakua hawapatani na mazao hayo

 Tumia pesticide kutibu magonjwa

 Tumia insecticide kuuwa wadudu waalibifu.

KUVUNA

Korosho hufikia hatua ya kuzaa matunda pale inapo kua na umri wa miaka 2 1/2 hadi 2. miaka mitatu.

Pia matunda ukomaa pale inapo kua na miaka 9 hadi 10

Uwezekano wa mkoroso kuishi ni miaka 30 hadi 40

Lakini pia kuvuna hua kunaanza mwezi october hadi mwezi december

MWISHO TUANGALIE MATUMIZI YA KOROSHO

Korosho hutumika kwa matumizi yafutayo;

Chakula

 Hutumika kutengeneza rangi

 Hutumika kama zao la biashara

 Miti yake hutumkia kama kuni

 Kutengeneza dawa

Post a Comment

0 Comments