
Mkulima anashauriwa kuhakikisha kuwa ana mtaji kabla hajaamua kufanya ufugaji wa samaki, kiwango cha mtaji kitategemea ukubwa wa mradi husika.
Soko
Ni vyema kujua upatikanaji wa soko pamoja na washindani wako kabla ya kuanzisha mradi huu, japo kwa nchi yetu soko la samaki ni kubwa sana, hii inatokana na uhitaji mkubwa wa samaki katika maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.
Elimu
Mkulima anapaswa kuwa na elimu ya kutosha kuhusu samaki na jinsi ya kufuga ili aweze kuendesha mradi kwa urahisi, hivyo mkulima anaweza kutafuta mtaalam kutoka vyuo vya serikali au binafsi na kuhudhuria semina mbalimbali zinazohusu ufugaji wa samaki.
Upatikanaji wa mbegu(vifaranga) pamoja na chakula.
Mkulima anashauriwa kuwa na uhakika wa upatikanaji wa mbegu bora ya samaki na chakula cha kutosha kwa ajili ya kulisha samaki.
Eneo la kufugia samaki
Ni vyema pia kutafuta eneo zuri kwa ajili ya kuchimba bwawa la kufugia samaki kwa kuzingatia upatikanaji wa maji kwa wakati wote wa msimu wa ufugaji, aina ya udongo, usalama na upatikanaji wa miundombinu husika (barabara, nishati ya umeme).
AINA YA SAMAKI;
Utafiti umefanyika katika nchi nyingi na ikaonekana kuwa samaki aina ya perege/ngege/sato [tilapia] na kambale (Catfish) wanafaa kufugwa katika mabwawa kulinganisha na aina nyingine.
Samaki wa aina hii wana sifa nzuri sana kwani;
huishi kwenye maji yenye joto la kadri katika nchi nyingi, wanaweza kuzaana kwa wingi katika mabwawa haswa sato), hula majani na chakula kingine chochote kinachopatikana kwa urahisi shambani au nyumbani, hukua kwa haraka, uvumilia sana changamoto za bwawa hii ikiwa ni mabadiliko ya joto, hewa ya oksijeni, na pH, pia nyama ya samaki hawa ni tamu na yenye ladha nzuri.
Kuna aina nyingi za sato(tilapia) kama vile Sato mwekundu, Sato wa Msumbiji, Sato mweupe na Sato wa Mwanza.
Sato hawa hula mimea na majani, hawaitaji chakula kingi na huzaana sana, wana doa moja kubwa kwenye pezi la mgongoni. Sato hawa hula vijimea vya plankiton, hukua kwa haraka na wana mistari kwenye mikia. Aina nyingine za samaki zimechanganyikana na kuwa machotara hivyo siyo rahisi kuwatambua.
Sato wa Mwanza ni moja kati ya aina ya tilapia inayoshairiwa kufugwa na wataalamu wengi kwa kuzingatia sifa mbalimbali tofauti na aina nyingine.
0 Comments