About Me

header ads

Ongezeko kodi ya majengo kupitia luku kuanza kesho


Na mwandishi wetu,Der-es-salaam

Wakati ulipaji wa kodi ya majengo kupitia manunuzi ya luku ukianza kesho, Ijumaa Agosti 20, 2021 kumekuwa na ongezeko la kodi hiyo kwa viwango tofauti.

Hiyo ikiwa na maana kuwa sasa walio na nyumba za kawaida ndani ya kiwanja kimoja watalipa Sh12, 000 kutoka Sh10, 000 iliyokuwa ikitozwa awali na Sh60, 000 kwa kila sakafu ya ghorofa kutoka Sh50, 000.

Kwa upande wa Halmashauri za Wilaya na Miji Midogo wao pia wataguswa na ongezeko hilo licha ya wao kuwa na ahueni kwani watalipa Sh60, 000 kwa nyumba za ghorofa bila kujali idadi ya sakafu

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Alphayo Kidata leo inaeleza kuwa utekelezaji huo unafanyika chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ukihusisha mita za aina zote za umeme.

Hili linafanyika kufuatia marekebisho ya Sheria ya Kodi ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa, Sura ya 289 iliyopitishwa na Bunge la Bajeti la mwaka 2021 ambapo viwango vya kodi ya majengo vimebadilishwa,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.


Post a Comment

0 Comments