About Me

header ads

Vita vya Afghanistan: Je, ni nani walio kwenye utawala wa Taliban?

Chanzo cha picha, Getty Images

Kundi la wapiganaji wa Taliban liliwashangaza wengi kwa kufanikiwa kuiteka nchi hiyo ndani ya siku kumi pekee. Na kuchukua kwa kasi miji na miji mikuu. Bado haijulikani ni nani atakayechukua uongozi wa serikali mpya . lakini ni kipi tunachojua kuhusu uongozi wa kundi hilo?

1. Hibatullah Akhundzada

Hibatullah Akhundzada ndiye aliyechukua uongozi wa kundi hilo mwezi Mei 2016. Miaka ya 80 , alishiriki katika vita vya kundi hilo dhidi ya jeshi la Usovieti nchini Afghanistan , lakini sifa yake ni zaidi ya ile ya kiongozi wa kidini badala ya kamanada wa jeshi la Taliban.

Akhundzada alifanya kazi kama mkuu wa mahakama za sharia katika miaka ya tisini. Baada ya kuchukua mamlaka miaka ya tisini , Kundi la taliban lilianzisha na kuunga mkono adhabu kulingana na sheria za Kiislamu : Waliuawa hadharani wauaji na wazinzi na kuwakata mikono wezi.

Chini ya uongozi wa Mullah Mohammed Omar ambaye anafikiriwa kufariki 2013 , Taliban walipiga marufuku runinga, muziki, filamu, vipodozi na kuwazuia wasichana walio na umri wa miaka 10 na zaidi kwenda shule.


Chanzo cha picha, EPA

Akhundzada anaaminika kuwa katika miaka yake ya sitini na ameishi Maisha yake mengi nchini Afghanistan, hatahivyo kulingana na wataalamu , ana uhusiano wa karibu

Hatahivyo, kulingana na wataalam, ana uhusiano wa karibu na kile kinachoitwa "Quetta Shura" - viongozi wa Taliban wa Afghanistan wanaosemekana wako katika mji wa Quetta nchini Pakistani.



Kama kamanda mkuu wa kikundi hicho, Akhundzada ndiye anayesimamia masuala ya kisiasa, jeshi na dini.


2. Abdul Ghani Baradar


Chanzo cha picha, Getty Images

Mullah Abdul Ghani Baradar ni mmoja wa watu wanne ambao walianzisha Taliban huko Afghanistan mnamo 1994.

Alikamatwa katika operesheni ya pamoja ya Marekani na Pakistani katika mji wa Karachi kusini mwa Pakistani mnamo Februari 2010.

Alikaa gerezani kwa miaka minane, hadi alipoachiliwa kama sehemu ya mpango wa kuwezesha mchakato wa amani. Amekuwa mkuu wa ofisi yao ya kisiasa nchini Qatar tangu Januari 2019.

Mnamo 2020, Baradar alikua kiongozi wa kwanza wa Taliban kuwasiliana moja kwa moja na rais wa Marekani baada ya kufanya mazungumzo ya simu na Donald Trump.

Leo, Abdul Ghani Baradar ndiye kiongozi mkuu wa kisiasa wa Taliban.

"Tumefanikiwa ushindi ambao haukutarajiwa ... sasa inahusu jinsi tunavyowahudumia na kuwalinda watu wetu," Baradar alisema katika taarifa iliyoandikwa huko Doha, mji mkuu wa Qatar, ambapo alikuwa sehemu ya timu ya mazungumzo ya Taliban ya mazungumzo ya amani.


Chanzo cha picha, Getty Images

3. Mohammad Yaqoob


Anaaminika kuwa na zaidi ya miaka 30 na kwa sasa ndiye kiongozi wa operesheni za jeshi la kikundi hicho.

Baada ya kifo cha kiongozi wa zamani wa Taliban Akhtar Mansour mnamo mwaka 2016, wanamgambo wengine walitaka kumteua Yaqoob kuwa kamanda mkuu wa kikundi hicho, lakini wengine walihisi kuwa alikuwa mdogo na hana uzoefu.

Kulingana na vyombo vya habari vya huko, Yaqoob anaishi Afghanistan.

4. Sirajuddin Haqqani

Sirajuddin Haqqani ni mmoja wa manaibu viongozi wakuu wa kikundi.

Baada ya kifo cha baba yake, Jalaluddin Haqqani, alikua kiongozi mpya wa mtandao wa Haqqani, ambao umetajwa kuwa na mashambulio makali zaidi ambayo yametokea Afghanistan dhidi ya vikosi vya Afghanistan na washirika wao wa Magharibi miaka ya hivi karibuni.

Mtandao wa Haqqani kwa sasa ni moja ya vikundi vya wanamgambo vyenye nguvu na wanaoogopwa. Wengine wanasema lina ushawishi zaidi kuliko kundi la Islamic State huko Afghanistan.

Chanzo cha picha, FBI

Haqqani anaaminika kuwa na umri wa miaka 45 na haijulikani alipo.

5. Abdul Hakeem

Mnamo Septemba 2020, Taliban ilimteua Abdul Hakeem kama mkuu mpya wa timu ya mazungumzo ya Taliban huko Doha.

Anaaminika kuwa na umri wa miaka 60. Aliripotiwa kuendesha madrassa - shule ya dini ya Kiislamu - huko Quetta, Pakistan, ambapo pia alisimamia mahakama ya Taliban.

Viongozi wengi waandamizi wa Taliban waliripotiwa kukimbilia Quetta, ambapo waliongoza kikundi hicho.

Lakini Islamabad imekanusha uwepo wa "Quetta Shura".

Hakeem pia anaongoza baraza lenye nguvu la wasomi wa dini la Taliban na anaaminika kuwa mmoja wa watu wa karibu na kamanda mkuu, Akhundzada.


NCHI NNE ZINAZOENDELEZA UHUSIANANO NA KUNDI HILO





Chanzo cha picha, Reuters

Huku Marekani na nchi nyingi za magharibi zikiharakisha kuwoandoa raia wake nchini Afghanistan baada ya kundi la Taliban kuuteka mji mkuu wa Kabul na kuchukua madaraka, kuna mataifa ambayo hayana wasi wasi wowote kuhusu kuendelea na uhusiano wao na watawala wapya wa Taliban .

Mataifa hayo yameonekana kutotikiswa na hofu ambayo Marekani na washirika wake wameonyesha baada ya Taliban kushika hatamu.

Miongoni mwa nchi hizo ni China ,Urusi ,Pakistan na Qatar. Mataifa hayo yamesema yataendelea na uhusiano wa kidiplomasia na Afghanistan na hata kulipa kundi hilo msaada linapoendelea na juhudi za kuunda serikali mpya nchini humo. Lakini kwanini nchi hizo zinaonekana kutokuwa na hofu kuhusu Taliban kuingia madarakani?

Urusi


Chanzo cha picha, Getty Images

Urusi imekuwa mshirika mkubwa wa Taliban, ingawa mara kadhaa imekana kuisaidia kwa silaha kundi hilo

Baada ya kuangushwa kwa serikali ya Afghanistani, kampeni ya kimya kimya ya kulifikia kundi la Taliban kama imemlipa Rais wa Urusi Vladimir Putin. Kwenye maandishi kundi hilo limepigwa marufuku na Moscow, na mpaka sasa Serikali ya Urusi haijasema lolote kama italitambua kundi hilo kama serikali halali ya Afghanistan.

Lakini kauli ya wiki hii Waziri wa masuala ya kigeni wa Urusi alitangaza kwamba Urusi imeanza mawasiliano na Taliban ambayo imesema "imeanza kurejesha hali ya utulivu" jijini Kabul na maeneo mengine ya Afghanistan. Wakati Taliban wakiuvamia mji wa Kabul huku vikosi vya jeshi la Marekani vinavyomuunga mkono Raiss Ashraf Ghani vikiondoka, warusi waliweka wazi kwamba hawataondoa shughui zao za kidiplomasia nchini humo.

Katika taarifa yao wamesema, ni kwa sababu Taliban wamechukua nchi bila kukutana na upinzani wowote kutoka kwa vikosi vyilivyofundishwa na Marekani na washirika wake. Kidiplomasia, Urusi kama inaiunga mkono Taliban, iliweza kuruhusu mkutano huko Moscow uliohudhuriwa na Taliban, mjumbe wa baraza kuu la usalama la Afghanistan na shirika la kijamii, na kuipaisha Taliban kimataifa.

Katika taarifa zingine zinasema kuwa, Taliban imekuwa ikipokea silaha zake kutoka Urusi, ingawa mara zote Urusi imekuwa ikikana kuwapa silaha wapiganaji wa kundi hilo.

China



Chanzo cha picha, Getty Images

China, ikiongozwa na waziri wake wa nje Wang Yi (kulia) iliwaalika wawakilishi wa Taliban kwa mazungumzoo huko Tianjin


Wakati Taliban ilipotawala kwa mara ya kwanza Afghanistan mwaka 1996, Chinailikataa kuutambua utawala huo na kufunga ofis zake za ubalozi kwa miaka kadhaa. Lakini kwa sasa Serikali ya China imekuwa nchi ya kwanza kuwakumbatia wanamgambo hao wa kiislamu.

Kigeugeu cha China kilionekana wiki mbili tu zilizopita, pale waziri wake wa kigeni Wang Yi alipoukaribisha ujumbe wa Taliban huko kaskazini mwa Tianjin, wakati huo wakiwa katika hatua za mwisho mwsho za kumuondosha madarakani Rais Ashraf Ghani, aliyetoroka nje ya nchi Jumapili ya wiki hii.

Wang akabariki kundi hilo kwa kusema "lina majukmu muhimu" ya kutawala Afghanistan kauli iliyozidi kuwapa nguvu Taliban na uhalali wa unachokifanya licha ya utawala wa kundi hilo kukosolewa na wengi ukitajwa kuendekeza ugaidi na kukandamiza wanawake.

China inahofia kuongezeka kwa uislamu wenye msimamo mklai miongoni mwa jamii ya wachina wachache wa Uyghur ambao wameonekana kuongezeka katika miaka ya hivi karibuni.

China pia inataka kuendelea kujiimarisha kichumi kupitia jamii ya kimataifa , ikiwa na uchumi wa $14.7 trillion — ambao ni mara 17 zaidi ya uchumi wake wa mwaka 1996 — ukishamirishwa na biashara za ndani nan je ya taifa hilo.

Lakini kuongezeka kwa uhasama kati ya Marekani na China, umefanya China kuendelea kujiimairsha yenyewe na kupunguza nguvu ya Marekani katika mataifa ambayo Marekani iliweka mizizi. Hilo ndilo linafanya kila fursa ikitokea Rais Xi Jinping wa China kuitumia kuwafurusha maadui zake, hasa Marekani wasiwakaribie wao na mipaka yake.

Haya ndiyo yanafanya China ionekana kama nchi kubwa itakayohodhi Afghanistan wakati huu Taliban ikijiandaa kutangaza taifa hilo kuwa taifa linalofuata misngiya kiislamu

Pakistan



Chanzo cha picha, USIP
 
Balozi Asad Majeed Khan wa Pakistani

Waziri mkuu wa Pakistani Imran Khan, alisema jumatatatu ya wiki hii kwamba Afghanistan imevunja na kuondoa pingu za utumwa, baada ya serikali ya nchi hiyo kusambaratika. MMoja wa mabalozi wenye nguvu Pakistani Asad Majeed Khan aliwahi kueleza kwenye mkutano wa masuala ya amani wa USIP, Julai 7, 2021 kwamba. "kuwekeza kwenye amani Afghanistan ni namna pekee ya kupunguza ugaidi unaoendelea". Lakini kushika hatamu kwa kundi la Taliban chini Afghanistan kuna maana gani kwa majirani zao Pakistani?

Kifuupi, Marekani na raia wengi wa Afghanistan wanachukizwa na kitendo cha Pakistan kuisapoti Taliban, hali hiyo ikateresha uhusiano wa Marekani na Pakistan. Kinachoelezwa ni kwamba ushindi wa Pakistan ni maslahi ya kimkakati kwa Pakiostan, ingawa maafisa wa Pakistan wamekuwa wakikana kuwa na maslahi yoyote.Ngawa bado makundi ya kigaidi yapo, Pakistan inaamini, itakuwa salama zaidi Taliban wakiwa madarakani kwa sababu ya nguvu yao kijeshi na uswahiba wao.

Kwa mujibu wa ripoti ya baraza la usalama la Umoja wa mataifa, kuna magaidi zaidi ya 6,000 wanaofanya kazi zao kutokea mpaka wa Afghanistan ambao wanaungwa ama wanashirikiana naTaliban. Kwa kuwa Taliban wanaungwa mkono na Pakistan, huenda Pakistan inajihisi iko salama kiasi.

Inaelezwa pia wapiganaji wa Taliban katika kipindi chote cha miaka 20 wamekuwa wakipatiwa matibabu Pakistan, ambayo kibiashara pia imekuwa na soko katika nchi ya Afghanistan na imekuwa ikitoa huduma kwa taifa hilo.

Qatar


Chanzo cha picha, Getty Images

Asila Wardak (kushoto) kutoka baraza kuu la usalama la Afghanistan na Anarkali Honaryar, mwanasiasa wakiwa Doha kwenye mkutano wa kusaka amani wa Taliban na Marekani uliofanyika Doha, Julai 7, 2019

Qatar imekuwa taifa muhimu kwa amani ya Afghanistan na imekuwa ikiendesha mazungumzo ya amani kati ya serikali iliyofurushwa na kundi la Taliban. Pia imekuwa nchi inayoiunga mkono Taliban wazi, ikielezwa kukisaidia kikundi hicho kiuchumi nakisiasa na kukipa hadhi ya kukitambua kimataifa.

Kwa Taliban kushika hatamu sasa Afghanistan, Qatar inaweza kuwa mnufaika wa kwanza baada ya Qatar kusimamia mazungumzo yaliyohusisha maafisa wa Marekani. Mazungumzo ambayo yamesaidia Marekani kuondoa vikosi vyake Afghanistan, kutolewa kwa wafungwa wa kisiasa na kivita katika magereza ya Afghanistan.

Baada ya Taliban kushika hatamu, kundi hilo linatarajiwa kupata msaada mkubwa wa kifedha kutoka Qatar ambayo nayo inatarajia kujiongezea nguvu katika maeneo ya Asia ya kati na maeneo mengine jirani kwa ajili ya shughuli zake za kiuchumi.

Post a Comment

0 Comments