About Me

header ads

Wajue wanyama 5 wa ajabu waliokuja na mageuzi kwenye maisha yao wanyama 5 wa ajabu waliokuja na mageuzi kwenye maisha yao


Kwa mujibu wa takwimu, kuna mamilioni ya wanyama duniani. Wanyama wanaotegemeana kwenye maisha. Wanyama wanaosihi maisha yao kwa kutegemea maisha ya wanyama wengine.


Wanyama wanaojilinda na kulinda wanyama wenzao, lakini aina zote za wanyama unazozijua duniani hazijitofautishi kwa namna ya walivyo kwa maana ya maumbo yao pekee, bali ni pamoja na tabia zao na mtindoi wao wa maisha.


Wapo wanyama waishio majini na nchi kavu ambao, mtindo wao wa maisha wanapotaka kuzaliana, kulea,kula ama kujilinda kunawatofautisha na wanyama wengine. Wapo wanyama wengi duniani ambao, wana ukuaji wa ajabu unaowafanya kuonekana ni wanyama wa kushangaza na wa ajabu, miongoni mwao ni hawa watano:


1. Invisible frog


Chanzo cha picha, Getty Images

Viumbe wengi wamekuwa wakificha viungo vyao, ama viungo vyao vya ndani havionekani vikifunikwa ama kuzibwa na tabaka nyingi za ngozi laini na nyembemba ama mifupa. Lakini inakuwaje kama tabaka hizi za ngozi zikiruhusu mtu kuona viungo karibu vyote vya ndani?

Jaribu kufikiria kuhusu dirisha la kiooo, unachoweza kuona mpaka ndani, sasa chura huyu unaona viungo vyake vyote vya ndani, ngozi yake ni kama kioo tu... unaona moyo wake unavyofanya kazi, mishipa yake ya damu inavyopitisha damu unaona kila kitu, unaona pia sehemu ya utumbo unaopitisha chakula kutoka mdomoni kwenye tumboni.

Amfibia huyu amekuwa na ngozi laini na nyembamba sana. Utaona kirahisi vitu vyake vya ndani kukiwa na mwanga kwa mfano wa jua.

Kwa mujibu wa watafiti vyura hawa wanapatikana zaidi kwenye misitu minene yenye mvua kubwa katikati na kusini mwa Amerika na wanatumia muda wao mwingi kwenye majani hasa mapana na umbo la vyura hawa wakiwa kwenye majani, inawafanya kuwa salama na ngumu kwa maadui wanayetaka kuwavamia kwa lengo la kuwadhuru, kwa mujibu wa utafiti.

2. Walking fish


Chanzo cha picha, Getty Images

Ni aina ya Samaki anayetembea maarufu kama Mexican walking fish na anajulikana pia kama axolotls, ambaye anakasi sana akiwa majini: Mbali na mwendo wake wa kawaida kama samaki wengine, lakini anajitofautisha nao kwa kuwa anaweza kutembea." Akiwa majini akikaribia kufika kwenye usawa wa ardhi ama kwenye miamba anatoa miguu yake minne na kuanza kutembeaa. Wanapatikana zaidi huko Mexico.

Ingawa wanaonekana kama samaki lakini kisayansi wanawekwa kwenye kundi moja la amfibia. Mara nyingi amfibia huanza maisha yao kwa kusaidiwa na matezi yao yanayowasaidia kwenye upumuaji wakiwa majini mpaka watakapokuwa na matezi hayo kuondoka, wanakuwa tayari kuanza maisha mengine nje ya maji(ardhini). Lakini kwa axolotls wamekuwa wakisalia na matezi yao na kubakia majini, Kwa mujibu wa chapisho moja la kisayansi kwenye jarida la Nature.

Kamwe hawatoki majini, axolotls unawakuta zaidi wenye ziwa Xochimilco karibu na Mexico City, wakikuwa hufikia urefu wa inchi 12 ama sentimeta 30. Wakiwa majini wanakula vijidudu vidogovidogo, konokono na minyoo. Kihistoria, viumbe hawa waikuwa wengi, lakini sasa wamepungua kwa sababu wamekuwa wakiliwa na samaki hasa aina ya tilapia na carp wanaopenda kula axolotls watoto. Upo wasiwasi wa viumbe hivi kupotea kabisa.

3. Pregnant males



Chanzo cha picha, Getty Images

Kwa tafsiri isiyo rasmi ya kiswahili, viumbe hivi vinaitwa farasi wa majini, kwa sababu ya muonekano wake ni kama farasi kabisa, sema ni wadogo kwa umbile. Maajabu ya viumbe hawa ni kwamba, Seahorse wa kiume ndiye hubeba mimba na kuzaa, kwa mujibu wa wanasayansi wa Marekani.

Viumbe hivi vinawahifadhi watoto wao wadogo kwenye vifuko maalumu kupitia vifuko hivyo huwapa watoto hao vyakula vya kuwapa nguvu. wakati mayai ya viumbe hivi hukaa kwenye mkiwa wa farasi wa majini wa kiume. Lengo ni kuwapa nafasi farasi wa kike kushughulika na utagaji wa mayai na kuacha majukumu mengine kwa farasi wa kiume, kwa sababu wanauwezo wa kuzaa asubuhi na kubeba mimba tena jioni, kwa mujibu wa National Geographic.

Frasi wa maji wakiume hubeba watoto kwa sababu wana nguvu, wakati wa kike wamekuwa na nguvu kidogo kwa sababu nguvu yao nyingi hutumika kutengeneza mayai, kuliko nguvu zinazotumika kwa wa kiume kutengeneza mbegu, hiyo ni kwa mujibu wa Oxford Academic. Baada ya kutengeneza mayai, farasi wa majini wa kike humpatia mayai wa kiume kwa ajili ya kuyabeba na kusaidia uchavushaji.

4. Anglerfish


Chanzo cha picha, Getty Images

Samaki hawa wa kiume na wa kike wamekuwa na muonekana tofauti tofauti kiasi kwamba unaweza kudhani ni aina tofauti ya samaki kumbe ni wale wale. Lakini Anglerfish wa kike ni mrefu mara 60 zaidi ya wa kiume lakini pia ana uzito mkuwa wa karibu nusu milioni ya uzito wa Anglerfish wa kiume; utofauti huu uliwafanya wanasayansi walivyokuwa wanamfuatilia anglerfish wa kike, walidhani kwamba samaki huyo alikuwa akimtafuta mwanae, kumbe ilikuwa tofauti, hiyo ni kwa mujibu wa American Society of Ichthyologists and Herpetologists.

Na alipofika Anglerfish wa kiume na kuanza kujamiana, Anglerfish huyu wa kiume akageuka na kuwa kama kimelea, kwa mujibu wa utafiti na kuanza kama kumng'ata na kung'ang'ania kwenye mwili mkubwa wa Anglerfish wa kike. Kwa sababu ya ukubwa na nguvu za Anglerfish wa kike, Anglerfish wa kiume hukaa tu, hafanyi chochote zaidi ya kutoa mbegu tu, shughuli zingine zote za kuwezesha tendo hilo hufanywa na Anglerfish wa kike. Baada ya tendo hilo, huzama majini kwa ajili ya uchavushaji na kupata watoto.

5. Immortal jellies



Chanzo cha picha, Getty Images

Ungetamani kurudisha umri nyuma na kurudi enzi zako za utoto? na kuanza maisha tena? Kadri muda unavyokwenda , miili ya binadamu imeumbwa kukua, na umri pia unaongezeka na baada mtu anafariki. Hata hivyo si kila kiumbe kinapitia hatua hizi. Kutana na Immortal jellyfish. Yeye ni tofauti.

Kiumbe huyu akiumia ama akikutana na hatari yoyote hujirudisha na kuanza upya maisha", kwa mujibu wa American Museum of Natural History (AMNH). jellyfish huanza maisha upya ya utoto., na kuendelea kukua tena . Wanasayansi wanasema , jellyfish mkubwa kabisa anafikia chini ya milimita 5. Kwa mara ya kwanza jellyfish wa aina hii waligunduika mwaka 1883 kwenye bahari ya Mediterranean, lakini walikuja kugundulika ama kuwa na mifumo inayofanya waendelee kuishi ilipofika miaka ya 1990s. Wanasayansi wanaendelea kuumiza kichwa kwa namna gani jellyfish amekuwa na maisha yasiyo na mwisho. 

Post a Comment

0 Comments